• Breaking News

  Oct 23, 2016

  CHADEMA imesema kesho mahakamani kupinga kile walichodai Dhulma katika Uchaguzi wa kumpata meya Kinondoni


  Chama cha demokrasia na Maendeleo Chadema kimesema kesho kinatarajia kwenda mahakamani kupinga kile walichodai Dhulma ililiyofanyika katika Uchaguzi wa kumpata meya wa manispaa ya Kinondoni kwa madai umefanyika kwa hila na kusababisha chama hicho kususia na Mgombea wa Ccm kutangazwa mshindi.

  M/kiti wa chama hicho Freeman mbowe akiwa amefuatana na wabunge mara baada ya kutoka nje ya ukumbi kususia Uchaguzio huo amedai kuwa Uchaguzi ulikuwa batili kutokana na sababu mbali mbali kama anavyoeleza.

  Katika hatua nyingine waandishi wa habari wa television na magazeti kutoka magazeti mbali mbali walizuiwa kuingia katika eneo la mktano na kutakiwa kukaa nje ya geti huku vyomvyo vya habari vichache vya vikiruhusiwa kushuhudia Uchaguzi huo.

  Afisa habari wa manispaa hiyo alipoulizwa na waandishi wa habari kutaka ufafanuzi wa kutoruhusiwa kuingia ndani alishindwa kutoa ufafanuzi na kudai kuwa ameagizwa kutoa zuio la waandishi habari kuingia ambapo pia mshindi wa Uchaguzi huo alitokea mlango wa mbele na baadhi ya wajumbe huku waandishi waliopo katika geti la kuingilia wakiachwa katika mataa.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku