• Breaking News

  Oct 5, 2016

  CHADEMA Wanakaribia Kuiua CUF Bara Kama Walivyofanya kwa NCCR

  Wadau, amani iwe kwenu.

  Kadri siku zinavyoenda tunazidi kuona mengi na inadhihirika rasmi kuwa UKAWA ulijengwa kwa msingi wa matofali ya barafu. Baada ya uchaguzi wa 2015, tumeshuhudia chama cha NCCR Mageuzi kikisambaratika kwa kupoteza wabunge wote wa Mkoa wa Kigoma. NCCR wakajikuta wanabaki na mbunge mmoja tu ambaye ni Mwenyekiti wake Francis Mbatia aliyeshinda jimbo la vunjo kwa mgongo wa CHADEMA.

  Baada ya uchaguzi huo, tumeshuhudia CUF wakijiimarisha Tanzania Bara kwa kushinda viti kadhaa vya wabunge. Pia wameshinda viti vya udiwani. Hii ni tofauti na uchaguzi wa 2010. Hali hii haijawafurahisha CHADEMA hata kidogo. Kuimarika kwa CUF maana yake ni kudhoofika kwa CHADEMA hasa katika maeneo ya Mikoa ya Mwambao.

  Ili kukabiliana na nguvu ya CUF, CHADEMA wametumia mbinu za DIVIDE AND RULE. Wamefanikiwa kuigawa CUF vipande viwili. Kwa upande wa Tanzania Bara, Julius Mtatiro ndiye anayetumiwa na CHADEMA kuwaua CUF. . Kwa upande wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad na watu walio karibu naye wapo mikononi mwa CHADEMA.

  Inadaiwa kuwa wafadhili wa CHADEMA ambao ni Taasisi ya KAS ya Ujerumani inawapa fedha viongozi hao na inagharamia shughuli zote za chama kutokana na uamuzi wao wa kususia uchaguzi mkuu wa marudio hali iliyosababisha wapoteze wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Maalim Seif kutokuwa Makamu wa Kwanza wa Rais. Inadaiwa kuwa taasisi hiyo ya KAS ndiyo iliyogharamia safari za viongozi wa CUF Jumuiya ya Ulaya na Marekani.

  Tukumbuke kuwa CHADEMA ilifanya hila ili CUF isifanikiwe kupata Meya kwenye Halmashauri walizoshinda. Hayo yametokea KInondoni na Temeke.
  Kinachoshangaza zaidi ni kwamba CUF hawajashtuka. Wapo viongozi wachache kama akina Magdalena Sakaya ambao wanaona jahazi linazama. Wanajaribu kufurukuta lakini hawaoni mwelekeo.

  CHADEMA wamewazunguka CUF kila kona. Wanaingilia mambo ya ndani ya chama ambayo hayawahusu. CHADEMA wanajaribu mpaka kuweka mawakili wakiongozwa na wanasheria wa chama hicho Tundu Lissu ili tu Prof Lipumba asifanikiwe kutwaa tena madaraka yake ya Mwenyekiti wa CUF.

  CUF inaelekea kuzimu. Karibuni watatumbukia kwenye shimo refu ambalo limejaa wadudu, wanyama na takataka hatarishi. Hawatapita salama. Hawatasalimika. Hata kama CHADEMA watafanikiwa kuwaondoa wale wanaoona hatarishi ndani ya CUF, haitakuwa na tija kwa CUF bali faida kwa CHADEMA. Ndio lengo lao kuu. Ili watakapoingia 2020, CUF isiaminike tena na iwe imepoteza wafuasi wake wengi. Mwisho wa siku, UKAWA utavunjika rasmi na CHADEMA itasimamisha wagombea kwenye majimbo yote. Mwisho wa siku CUF kitakufa.

  Nawahurumia sana CUF. Laiti wangalijua unafiki wa viongozi wa CHADEMA wasingalithubutu hata kuwaalika sebuleni.

  Imeandikwa na Lizaboni/Jamii Forums

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku