• Breaking News

  Oct 1, 2016

  CHADEMA Yafuta Rasmi Maandamano ya UKUTA, Yatangaza Mbinu Mpya ya Kudai Demokrasia

  Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, hatimaye leo kimetangaza kufuta rasmi maandamano na mikutano ya hadhara iliyokuwa imepewa jina la UKUTA.

  Badala ya maandamano hayo, CHADEMA kimeamua kutumia mbinu nyingine walizozitaja kuwa bora zaidi za kufikisha ujumbe waliokusudia kufikisha kwa serikali.

  Akizngumza na wanahabari Mwenyekiti wa Chadema Taifa. Mh. Freeman Mbowe, amesema, baada ya kusogeza mbele maandamano hayo na kuwapa nafasi viongozi wa dini kulifanyia kazi suala hilo hatimaye wamegundua kuwa hakuna chochote kilichofanyika.

  Amesema, suala la kudai haki za msingi siyo la siku moja hivyo, fikra za kudai haki na oparesheni UKUTA zinaendelea kudumu kwa kutumia mbinu nyingine mpya ya kufanya vikao nchi nzima na ziara za nje ya nchi ambapo ziara ya kwanza itakuwa nchini za Denmark, Ujerumani na Mataifa yanayojihusisha na masuala ya haki za binadamu.

  Aidha Mhe. Mbowe amewataka wanachama na wafuasi wa chama hicho kupuuza maneno ya siasa yanayoendeshwa na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba kutokana ba mgogoro ndani ya cha hicho huku akisema kuwa CHADEMA haimtambui Prof. Lipumba kama mwenyekiti wa CUF, na kwamba haitampa ushirikiano wowote.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku