• Breaking News

  Oct 11, 2016

  DC Hapi Aamuru Kuchunguzwa Mfanyabiashara Anayedaiwa Kusema ‘Serikali iko Mfukoni Mwake’

  Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Salum Hapileo asubuhi amewatembelea wananchi wa Tegeta kwa ndevu eneo ambalo baadhi ya wananchi walionekana kwenye vyombo vya habari wakilalamika kuhusu  kufanyiwa hila na mfanyabiashara mmoja ajulikanae kwa jina la Emily Reshea aliyechimba shimo mbele ya nyumba za watu na kuziba njia za wananchi kupita kama mbinu ya kuwalazimisha wamuuzie maeneo yao.

  Hapi akiwa katika eneo hilo akiambatana na wataalamu wa mipango miji, mhandisi wa manispaa na askari wa jeshi la polisi  ameagiza kuvunjwa kwa ukuta ulioziba njia za wananchi kupita, kufukiwa kwa shimo lililochimbwa kabla ya saa 12 jioni leo october 10 2016 na kumtaka OCD Kawe kuchunguza tuhuma za mfanyabiashara huyo kudaiwa kusema kuwa  “serikali iko mfukoni mwake” na ikibainika kuwa ni kweli akamatwe mara moja na kuhojiwa na vyombo vya dola.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku