Oct 9, 2016

DONALD Trump Kufichua Uhusiano wa Kimapenzi wa Clinton

Mshauri mmoja wa mgombea wa urais nchini Marekani Donald Trump ,amesema kuwa mfanyibiashara huyo bilionea huenda akatumia mjadala wa kesho Jumatatu kuzua historia ya uhusiano wa kimapenzi wa Bill Clinton.

Rudy Giuliani amesema kuwa Trump na Hillary wana maswala katika maisha yao ya kibinafsi ambayo ni ya aibu.
Alikuwa akijibu hisia kali zilizojiri dhidi ya Trump baada ya madai ya kuwatusi wanawake.

Bwana Trump amepoteza uungwaji mkono wa zaidi ya viongozi 20 wa chama cha Republican ,wengi ambao wanamtaka ajiondoe katika kinyang'anyiro cha urais baada ya kuzuka kwa rekodi za muongo mmoja ambapo amekuwa akijisifu kuwatumia kimapenzi wanawake

Install SIASA HURU App Kwenye Simu Yako Kusoma Habari hizi Kirahisi, Bonyeza HAPA

Post a Comment

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © Siasa Huru l Habari za Siasa | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by SiasaHuru.com