• Breaking News

  Oct 19, 2016

  Hakuna Siku Nimejisikia Uchungu Mkubwa Kama Jana, Kwasababu Nafahamu Historia ya Mradi wa Hospitali ya Mama na Mtoto

  Hakuna siku nimejisikia uchungu mkubwa kama jana, kwasababu nafahamu historia ya Mradi wa Hospitali ya Mama na Mtoto, na nimeshiriki katika hatua mbalimbali za ujenzi wa maono haya.

  Lema alikuwa na ndoto hii kwa muda mrefu, na aliitangaza hadharani katika kampeni zake na CCM walimdharau na kumuona kichaa, na wakati mwingine Lema alikuwa akisema, CCM wakiendelea kumuudhi na kumkejeli na ndoto hiyo, ataijenga hiyo hospitali na ataiwekea na swimming pool mithili ya hotel.

  Muda ukafika Lema kupitia ushawishi wake na timu yake wakafanikiwa kupewa kiwanja na Mawala Trust, na siku ya makabidhiano nilikuwepo, na hakukuwepo kiongozi yeyote wa Serikali, Mgeni rasmi alikuwa Mh. Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chadema.

  Hii inaonesha wazi kabisa Mawala si tu walikuwa na moyo wa kusaidia watu wa Arusha kupata Hospitali ya kusaidia akina mama na watoto, pia walionesha mapenzi ya wazi kwa Chadema, kwa kukabidhi kiwanja hicho chini ya Ugeni Rasmi wa Mwenyekiti wa Chadema taifa.

  Hatua iliyofuata ilikuwa ni kutafuta udhamini wa ujenzi wa Hospitali hiyo kitu ambacho watu wa Arusha tulisema hata kwa michango binafsi tutaweza kuchangia ujenzi wa hospital hiyo, lakini Mh. Mbunge kwa ushirikiano na taasisi yake ya Arusha development Foundation (ArDF) waliendelea kutafuta wahisani hadi walipokutana na watu wa Maternity Afrika ambao waliingia nao mkataba wa kujenga Hospital hiyo kwa thamani ya Bilioni 9 za Kitanzania.

  Hatua ya aibu ni ya leo ambayo huyu anayejiita mkuu wa mkoa kutaka kwa makusudi kuharibu kazi nzuri iliyofanywa kwa miaka mingi bila msaada wowote wa serikali, kisa ameitwa tu kuiwakilisha serikali kama mgeni rasmi, tena Lema akiwa hana shida yoyote ya uwepo wake.

  Aina hii ya viongozi hawawezi kutufikisha kwenye nchi ya viwanda anayosema Magufuli. Wamejaa ujinga wa kichama na wanafikiria muda wote ni muda wa kufanya siasa na kutweza kazi nzuri zinazofanywa na wapinzani.

  I find this to be the highest level of stupidity I have ever seen in a leader. It is so sad indeed.

  Vielelezo vya picha vipo hapo, na katika hatua zote hizi muhimu hajawahi kuwepo kiongozi wa serikali hii ya CCM, hadi Leo ndo wanajitokeza na maelezo yao binafsi yasiyo na mkia wala kichwa.

  By Emma

  1 comment:

  1. Na hiyo lugha aliyoitoa hapo ni ya kiongozi au mwakilishi wa watu??? Angalau RC kaonyesha busara ya kutoropoka upuuzi ati mtu yeyote anayepingana au kupishana na Lema basi JPM humpandisha cheo
   Ukisoma barua ya mwaliko kwa mgeni rasmi ambaye ni RC ni ishara ya wafadhili kuitambua serikali kitu ambacho Lema na chadema siku zote wamekuwa wakimimina matusi kwa lolote ni wazi kwa akili ya Lema hata kama ni raisi angekuwa ndo mgeni rasmi angeropoka vilevile
   Ni aibu sana

   ReplyDelete

  Siasa

  Michezo

  Udaku