• Breaking News

  Oct 19, 2016

  Hili la Arusha Linahitaji Mjadala Mpana, Ukisoma Barua ya Wafadhili Utajifunza Mengi

  Wafadhili wa mradi walimkaribisha Mkuu wa mkoa wa.Arusha, Mrisho Gambo kuwa Mgeni rasmi katika hafla ya jana (barua yaonyesha). Barua inaonyesha kuwa wafadhili si wanasiasa na wanatambua umuhimu wa Serikali katika kufanikisha mradi huo wenye manufaa kwa mama na mtoto.

  Mheshimiwa Godbless Lema alikuwa miongoni mwa wageni kadhaa waalikwa na hasa ikizingatiwa kuwa ni miongoni mwa waasisi wa mradi huo.

  Je, ile tafrani iliyotokea jana ni kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi, kuweka sawa rekodi za mradi ulivyoanza, kumtambua kwa kumtaja Mheshimiwa Mbunge kama mwasisi wa mradi, tu au kuna la zaidi ambalo jamii hailifahamu?

  Je, na njia iliyotumika kufikisha ujumbe ndio sahihi na inatoa picha gani kwa jamii kuhusu hekima ya uongozi?

  Wadau, tujadili pasipo kutumia lugha ya kashfa.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku