Oct 6, 2016

HISTORIA Fupi ya Scorpion Mtoa Macho Inayozunguka Mitandaoni

Alivyokuwa mdogo alikataa kusoma mama yake mzazi alishafariki siku nyingi na alikuwa akilelewa na mama yake mdogo maeneo ya Yombo buza.

Alishawahi kufungwa jela japo haijajulikana alikosa nini, na jina lake kamili ni Salum Njwope na jina hilo nila babu yake. Yeye ni mwenyeji wa mkoa wa Shinyanga. Kwa mujibu wa mama yake mdogo anasema Scorpio alipokua akitoka nyumbani usiku saa mbili anamuaga mama yake mdogo huyo kuwa anakwenda kwenye kazi ya ubaunsa katika club kumbe mwenzie alikuwa anaenda Buguruni kuibia watu mpaka asubuhi ndio anarudi nyumbani.

Pia scorpion ashawahi kushiriki katika shindano lililojulikana kama Dume Challenge kama miaka mitatu iliyopita na aliibuka mshindi. Napia alianza mafunzo ya kucheza caret tangu akiwa mdogo sana napia ni mtu mwenye nguvu za kuzaliwa nazo.

Kuna kipindi aliondoka nyumbani kwao kwa muda mrefu mama yake mdogo anadai alikuwa hajui yuko wapi mpaka baadae aliporudi mwenyewe nyumbani.

Amekamatwa na Polisi baada ya kutuhumiwa kumjeruhi mkazi mmoja wa Dar es Salaam eneo la Buguruni kwa kumng’oa macho katika kitendo kilichoelezwa kuwa ni wizi wa fedha.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR