• Breaking News

  Oct 16, 2016

  Issue ya Mikopo ya Elimu ya Juu itamharibia sana JPM

  Vyuo vya elimu ya juu vimefunguliwa huku wanafunzi wengi wakiwa njiapanda kuhusu mikopo yao ya ada pamoja na chakula na malazi. Suala la means testing kwa mwaka huu limekuwa tight sana kiasi kwamba kuna wanaojuta kuomba kudahiliwa na vyuo kwa sababu hata ule mkopo wa chakula na malazi hawapewi wengi wao na huwezi kusajiliwa chuoni bila kulipa angalau ada ya semester moja!

  Serikali inasema inaweka kipaombele kwa baadhi ya kozi/fani,fine bt ni asilimia ndogo saaana ya wanafunzi wanaochukua fani hizo za kipaombele ukilinganishwa na wengine,haiwezekani wooote wasome Petroleum Engineering,architechture,medicine,anatomy, and the like!

  Na wengi wa watoto wa maskini ndo hawa waliosomea shule za Kayumba ambako Physics na Biology ni msamiati mgumu sana so walilazimika kusoma masomo ya arts ili waweze kufaulu kwa sababu ya kukosa walimu wa sayansi na miundombinu ya maabara.

  Nionavyo mm,pesa nyingi inatumika zaidi huku kwenye 'ELIMU BURE',hali ikiwa mbaya zaidi hawa wanafunzi wa elimu ya juu wanaweza kugoma na hii itamletea shida kubwa sana JPM. Naomba washauri wake mliopo humu #JF mumfikishie salamu hizi,watoto wengi wa maskini ndo waliosoma masomo ya arts na ndo wanaokosa mikopo.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku