• Breaking News

  Oct 17, 2016

  Jacqueline si Mtoto wa Prof Ndalichako, Asihukumiwe Bila Hatia

  Baada ya kusambaa kwa taarifa inayoonesha wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2016/17 kumejitokeza mjadala mkubwa juu ya jina la binti aliyejulikana kama Jacqueline Ndalichako, akidaiwa kuwa mtoto wa Waziri wa Elimu Prof.Joyce Ndalichako.

  Mimi ni miongoni mwa watu waliohamaki baada ya kupata taarifa hiyo, na nikasema IKIWA NI KWELI JACQUELINE NI MTOTO WA PROF.NDALICHAKO basi inabidi Waziri huyo ajiuzulu. Hii ni kutokana na ukweli kwamba mtoto wa waziri hawezi kupata mkopo hata kama anakidhi vigezo vya kitaaluma. Mwongozo wa HESLB unamtaka mwanafunzi awe anatoka familia isiyojiweza kiuchumi, lakini mtoto wa Waziri hawezi kuwa kundi la wasiojiweza kiuchumi. Wapo watanzania wengi wenye uhitaji wa mikopo ya elimu ya juu kuliko watoto wa mawaziri.

  #UKWELI_KUHUSU_TAARIFA_HIYO.

  Baada ya kufuatilia nimegundua mambo yafuatayo:

  1. Jacqueline si mtoto, ndugu wala hana unasaba wowote na Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi. Ni ufanano tu wa majina, baina ya watu hawa wawili lakini ni watu wasiofahamiana kabisa.

  2. Profesa Ndalichako hana mtoto mwenye jina Jacqueline, wala hana ndugu mwenye mtoto mwenye jina hilo.

  3. Watoto wa Profesa Ndalichako walishahitimu elimu ya juu na hakuna yeyote anayejiunga na elimu ya juu kwa sasa.

  4. Jacqueline amehusishwa na Prof.Ndalichako kwa sababu ya ufanano wa majina, lakini si watu wenye kufanana nasaba.

  5. Jacqueline hakusoma HGL kama ilivyoelezwa. Amesoma EGM na amechaguliwa kusoma Shahada ya Uchumi na Takwimu (B.A in Economics and Statistics).

  6. Jacqueline anatoka familia yenye uchumi wa kawaida hivyo anakidhi vigezo vya kupewa mkopo. Amesoma St.Mary Gorreti katika mazingira ambayo si vzr kuyaeleza hapa. (Nimefuatilia taarifa za familia ya Jacqueline inayoishi Yombo Dovya lakini nisingependa kuziweka hapa).

  SWALI: Je waliosema Ndalichako awajibike wamekosea?

  JIBU: Hapana. Hoja ilikuwa "Kama kweli Jacqueline ni mtoto wake basi awajibike". Hii ina maana kuwa hakukuwa na sababu ya kuwajibika kama si mwanae.

  SWALI: Walioibua hoja ya Jacqueline kuwa mtoto wa Ndalichako wamekosea?

  JIBU: Ndio. Walioanzisha hoja hii wamekosea kwa kuwa kuna viashiria kwamba walikusudia kupotosha. Hoja hii imepata nguvu mitandaoni na kusababisha usumbufu ambao ungeweza kuepukika.

  #MyTAKE:
  Kwanza niwape pole Jacqueline pamoja na Prof.Ndalichako kwa usumbufu ambao kila mmoja ameupata.

  Pili niwatake wote wanaoendelea kusambaza taarifa kuwa Jacqueline na Prof.Ndalichako ni ndugu waache kufanya hivyo maana wanaweza kupotosha wengine.

  Ufanano wa majina si kigezo cha kuhukumu wasio na hatia pasipo uchunguzi. Bahati mbaya Jacqueline ameingia kwenye mijadala ya mitandao bila hatia. Amekuwa victim wa social media kwa sababu za kisiasa, ambazo yeye hahusiki nazo kabisa. Pia nimpe pole Prof.Ndalichako kwa usumbufu alioupata.

  Ukweli ni kwamba kufanana majina ni jambo la kawaida katika tasnia yoyote. Wapo wanafunzi wengi waliopo vyuoni au waliochaguliwa kujiunga na vyuo vikuu wenye majina yanayofanana na viongozi wakubwa kisiasa lakini hawajahusishwa na viongozi hao.

  Kuna mwanafunzi amechaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu Dodoma mwenye jina Gideon Wassira, lakini sijasikia akihusishwa na Mzee Stephen Wassira. Kijana Nobert Mbowe amehitimu Chuo kikuu Mlimani akisomea shahada ya Uhandisi wa madini (Mining Engineering) lakini hajawahi kuhusishwa na Mhe.Freeman Mbowe. Kuna mwanafunzi anaitwa Kennedy Yusuf Ndugai amechaguliwa shahada ya elimu maalum UDOM lakini hajahusishwa unasaba wake na Spika Job Ndugai.

  Kwa hiyo nitoe wito watu waache kutumia habari inayomhusu Jacqueline kwa kumhusisha na Waziri Ndalichako maana ni watu wasio na uhusiano wowote kinasaba.

  Najua wengi wamehamaki kusikia Jacqueline ni mtoto wa Waziri halafu kapewa mkopo huku watoto wa maskini wakikosa mikopo. Kumbe Jacqueline naye ni mtoto wa maskini pia, ila ameponzwa na ufanano wa majina na Waziri Ndalichako.

  Nihitimishe mjadala huu kwa kutoa rai kwa "bloggers &social media emperors" kutokuendelea kujadili suala la Jacqueline na Waziri Ndalichako maana ni watu wasiofahamiana kabisa, achilia mbali kuhusiana kinasaba. Tumpe nafasi Jacqueline aweze kucocentrate ktk masomo yake, asiwe frustruted na mitandao. Let us end this discussion to save this innocent poor soul.!

  Malisa GJ

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku