Oct 30, 2016

Jaji Mutungi Amuonya Maalim Seif

Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi amemuonya Katibu mkuu wa CUF Maalim Seif Sharrif Hamad kuacha kuvuruga chama cha CUF kwa maslahi yake.

Akizungumza kwa njia ya simu Jaji Mutungi amesema uamuzi alioutoa kuhusu CUF ulikuwa muafaka na laiti kama Maalim Seif angetii basi mgogoro ndani ya chama hicho ungekuwa umeshaisha.

Msajili huyo amesema kwa sasa anaangalia tu lakini akaonya atakichukulia hatua kali chama hicho kikiendeleza ukaidi wake na kama itafika mahali makundi ndani ya chama hicho yakionekana kuhatarisha amani ya nchi.

Kuhusu kwamba anatumika na CCM kuhujumu chama cha CUF msajili huyo amesema maneno hayo yanaenezwa na wapumbavu walioishiwa hoja na akasisitiza hata waseme nini Lipumba ndiye Mwenyekiti halali wa chama hicho mpaka mwaka 2019

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR