• Breaking News

  Oct 28, 2016

  Jecha Ndiye Aliikwamisha Nchi – Maalim Seif

  Wakati leo ni mwaka mmoja tangu matokeo ya Uchaguzi Mkuu Zanzibar yafutwe Oktoba 28, 2015, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amemtuhumu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kuwa ndiye aliikwamisha nchi kwa kupindua uamuzi wa wananchi.

  Maalim Seif alisema kutokana na uamuzi huo, ndiyo maana mpaka sasa mwenyekiti huyo ameshindwa kuibuka hadharani akielewa alibeba dhima ya Wazanzibari na Watanzania wote wapenda amani.

  Alisema hayo jana alipofanya ziara ya siku moja kwenye wilaya zote saba za Unguja ikiwa ni kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu Jecha alipofuta uchaguzi huo.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku