Oct 6, 2016

JENERALI Ulimwengu Afikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni Kusomewa Mashtaka Yanayomkabili

Mwandishi wa habari mkongwe nchini, Jenerali Ulimwengu (68), amesomewa mashitaka yake mbele ya Hakimu Issa Kasailo wa Mahakama ya Hakimu mkazi Kinondoni, Wakili wa Serikali, Matarasa Maharagande yaliyodai kwamba mtuhumiwa huyo alisababisha ajali hiyo Agosti 26 mwaka huu katika makutano ya barabara ya Kaunda na Ally Hassani Mwinyi Manispaa ya Kinondoni.

Alidai mtuhumiwa anakabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni kusababisha ajali na kumsababishia majeraha Irfan Merali, kutokana na kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha uharibifu wa magari mawili.

Alidai kuwa mshtakiwa akiwa dereva wa gari lenye namba za usajili T640 BEX  Mercedes Benz aliendesha katika barabara ya umma bila kuchukua hadhari ambapo alikatisha na kisha kugonga gari nyingine yenye namba za usajili T 470 DDS Subaru Preza ambapo baada ya kugonga gari hilo alimsababishia maumivu mtu aitwaye Irfan Montazir Merali aliyekuwa dereva.

Baada ya maelezo hayo mtuhumiwa alikiri kosa ambapo mahakama ilimtia hatiani kwa makosa hayo.

Kutokana na hatua hiyo, Mahakama ilimtaka mshtakiwa kulipa faini ya Sh 50, 000 au kwenda jela miezi sita. Na mwishoni Jenerali Ulimwengu alilipa faini hiyo. – Mtanzania

JENERALI ULIMWENGU AFIKISHWA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KINONDONI KUSOMEWA MASHTAKA YANAYOMKABILI

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR