• Breaking News

  Oct 15, 2016

  Jinsi ya Kujua Kama Simu Yako Imeingiliwa na Mtu Anakuchunguza Kwa Siri

  Kama una hofu kuwa kuna mtu anakufuatilia kwa siri au anakuchunguza (spying) kwenye simu yako, hauko mwenyewe. Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na idadi kuwa ya watu wakilalamika kuwa wamekuwa wakifuatiliwa katika simu zao bila ridhaa yao na bila wao kujua.

  Lakini kwa upande mwingine ni kuwa, kuna jinsi unaweza kufanya au ishara ambazo ukiziona zinakuonyesha moja kwa moja kuwa simu yako imeingiliwa na kuwa kuna mtu anakuchnguza kwa siri.

  Kufahamu viashiria hivyo, twende wote hadi mwisho wa makala hii.

  1. Kama betri ya simu yako inaisha chaji haraka kuliko kawaida, chunguza huenda kuna programu inayojiendesha bila ya wewe kujua.


  Kama kwenye simu yako hauna ‘games’ nyingi ambazo ukicheza mara kwa mara zinasababisha betri ya simu yako kuisha haraka, basi huenda sababu ni programu inayochunguza simu yako. Wakati mwingine simu huchukua muda mrefu kuchaji, hii ni kutokana na sababu kuwa wakati wewe umeweka simu chini unachaji, programu inayokuchunguza kwenye simu yako, inafanya kazi.

  2. Kama simu yako huwa ya moto wakati wote.

  Simu mara nyingi hupata moto inapokuwa inatumika, sasa kama simu yako umeiweka tu mfukoni au mezani lakini ukija unakuta ina moto kiasi kwamba unaweza kuchemsha yai, kutakuwa na programu zinazojiendesha kwenye simu yako. Kupata joto huku hakuhusiani na wakati wa kuchaji sababu simu nyingine hupata moto wakati zinachajiwa.

  3. Kama wakati unaongea na simu unasikia kelele za ajabu au mwangwi hata kama unayeongea naye yupo sehemu tulivu.

  Kama hali hii haikuwapo awali, yaani kama ulikuwa unaongea na simu kawaida lakini ghafla ukiongea unasikia kelele za ajabu na mwangi, huenda simu yako ina programu zinazojiendesha ndani ambazo hutumika kukuchaunguza wewe kwenye simu yako.

  Kama utaona dalili moja kati ya hizo kwenye simu yako, unaweza kupakua ‘Anti-spyware applications’ ambazo zitakuwasaidia kuilinda simu yako pasiwepo na programu zinazojiendesha zenyewe bila ridhaa yako na zikatumika kukuchunguza.

  JINSI YA KUJUA KAMA SIMU YAKO IMEINGILIWA NA MTU ANAKUCHUNGUZA (SPY) KWA SIRI

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku