• Breaking News

  Oct 16, 2016

  Kila Nipatapo Nafasi Kazi Yangu ni Kufunga-Kichuya

  Mshambuliaji wa timu ya Simba anayeongoza kwa kufunga magoli 7 katika mechi 9 alizocheza ligi kuu Tanzania bara msimu huu Shiza Kichuya amesema kila atakapo pata nafasi kazi yake ni kufunga.

  Kichuya ameyasema hayo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam baada ya kumalizika kwa mchezso kati ya Simba na Kagera Sugar mtanange ambao umemalizika kwa Simba kuibuka kidedea kwa kuicharaza Kagera Sugara bakoran 2 kwa bila.

  “Wachezaji kazi yetu ni kufunga, na mimi kila nitakapopata nafasi kazi ni kufunga na lengo letu ni kuendelea kuwa wamoja kama ilivyo sasa ambapo mashabiki pamoja na viongozi na wachezaji tupo wamoja ndiyo maana hata matokeo yanaonekana” Amesema Kichuya

  Wakati huo huo Nahodha wa Kagera Sugar George Kavila amesema Simba imepata nafasi na kuzitumia vizuri ndiyo maana wakaweza kuibuka na ushindi huo

  “Ligi hii ni ngumu huwezi kusema wameshinda kwa bahati, wamepata nafasi wakazitumia tutaenda kujipanga vizuri kwa michezo inayofuata” Amesema Kavila

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku