• Breaking News

  Oct 6, 2016

  KIMENUKA Kenya Watu Sita Wauwawa Kenya na al-Shabaab

  Watu sita wameuwawa nchini Kenya katika shambulizi linalohisiwa kufanywa na kundi la al-Shabaab.

  Watu sita wameuwawa nchini Kenya katika shambulizi linalohisiwa kufanywa na kundi la al-Shabaab katika eneo la makazi la Bulla katika mji wa Mandera.

  Tukio hilo limetokea majira ya saa nane usiku wa kuamkia leo wakati wapangaji wa eneo hilo wakiwa wamelala, ambapo polisi walifanikiwa kuwaokoa watu 25.

  Polisi wamesema washambualiaji hao waliwafyatulia hovyo risasi wapangaji wa makazi hayo baada ya kuvunja na kuingia kwenye makazi hayo.

  Kundi hilo la wavamizi lilitumia bomo la mkono kuvunja na kuingia katika makazi hayo na kisha kuwafyatulia risasi watu waliolala na baadaye kutoroka.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku