Oct 8, 2016

Kipa Ivo Mapunda Adai Atastaafu Kucheza Soka Siku Akisikia Robert Mugabe Amestaafu Siasa

Kipa mkongwe nchini aliyewahi kukipiga katika timu za Moro United, Yanga na Simba, Ivo Mapunda, amesema atastaafu kucheza soka siku akisikia Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe ametoka madarakani.

Ivo ambaye anasubiri kwenda kucheza soka Kenya, amesema kwa sasa hana kabisa mawazo ya kustaafu soka kama ilivyo kwa Rais Mugabe ambaye tangu aingie madarakani Desemba 22, 1987, mpaka leo bado ni rais wa nchi hiyo.

Mlinda mlango huyo, pia amewahi kucheza Gor Mahia ya Kenya na Saint George ya Ethiopia.


Ivo alisema bado nguvu anazo, hivyo akistaafu soka kwa sasa atakuwa hajakitendea haki kipaji chake, sasa anasubiri simu kutoka Kenya aende akacheze soka.“Labda watu wanaotaka kujua nitastaafu lini, niwaambie tu wasubiri siku wakimuona Mugabe anaachia madaraka ndiyo na mimi hapo hapo nitaacha kucheza soka,” alisema Ivo.

Mugabe ndiye rais anaongoza kukaa kwa muda mwingi zaidi madarakani huku akiendeleza ubabe bila ya woga hata kwa nchi za Magharibi.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR