• Breaking News

  Oct 7, 2016

  KR Muller kumtafuta Juma Nature ili kumaliza tofauti zao


  KR Muller ambaye kwa sasa ni member wa Rada Entertainment anajipanga kumtafuta kiongozi wa TMK Wanaume Halisi, Juma Nature ili kumaliza tofauti zao.

  Juma Nature amekuwa akimtuhumu KR kuaribikiwa baada ya kuhama TMK na kuhamia Rada Entertainment ya TID.

   KR amesema anajipanga kumtafuta Juma Nature ili kuzungumzia yaliyotokea.

  “Kusema kweli haya mambo yameniharibia sana, kuna wakati wazazi wangu baada ya kusikia nimeokotwa nikiwa nimelewa chakari walijisikia vibaya sana,” alisema KR. “Sijaonana na Juma Nature kwa muda mrefu, lakini napanga kumtafuta ili tuzungumze kwa sababu sisi tumetoka mbali,”

  Rapa huyo amesema kwa sasa anafurahia maisha mapya ndani ya label ya TID, Rada Entertainmet.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku