Wikiendi iliyopita msanii wa kimataifa kutoka Marekani Chris Brown alitua nchini Kenya na kufanya show katika tamasha la 'Mombasa Rocks Festival'

Katika show hiyo, alisindikizwa na wasanii kama Wizkid kutoka Nigeria, Alikiba kutoka Tanzania, Vanessa Mdee kutoka Tanzania na baadhi ya wasanii kutoka nchini Kenya na Uganda.

Katika show hiyo msanii huyo maarufu kutoka Marekani Chris Brown alionekana akiimba kwa kufuatiliza CD yaani 'Playback' na si kufanya muziki 'live' jambo ambalo limemfanya mwanamuziki Rama Dee kutoka Tanzania kuonesha kuwa hakupenda kile alichofanya msanii huyo mkubwa.
Rama Dee kupitia ukurasa wake wa Instagram alindika na kuwataka watu wa Afrika kushtuka kwani yeye hajapendezwa kabisa na kile alichofanya Chris Brown kwenda kuimba kwa kuifuatiliza CD nyuma ili hali inafahamika kuwa yule ni msanii wa kimataifa, hivyo alipaswa kuonesha utofauti mkubwa katika kufanya show.

"Huyu naye kaenda Mombasa kaweka 'CD' kaanza kuimbia juu. Ndiyo msanii wa kimataifa huyu? Tuamke waafrika jamani" aliandika Rama Dee


Post a Comment

 
Top