• Breaking News

  Oct 15, 2016

  Lowassa, Lipumba na Slaa waunde Chama Kimoja!

  Kuna kila dalili kua ukaaji wa Lowasa Chadema sio wa kudumu, unategemea tu kama some factors na kama hazitakuwepo, definitely ataondoka!

  Lipumba naye nia yake ya kuendelea kusikilia hapo buguruni, unaweza kukatizwa muda wowote! Kama baadhi ya mambo hayatakwenda sawa!

  Slaa naye, baada ya kupumzika vya kutosha huko Canada, nadhani ameshakusanya materials ya kutosha kurudi kwa spidi yake ya awali, hii ni baada ya kuoneshwa mlango wa kutokea pale chadema baada ya kutoridhishwa na baadhi ya mambo!

  Wanasiasa hawa watatu wanafanana sana katika mambo haya;

  1. Wanauzoefu wa kutosha wa siasa za Tanzania.

  2. Wana wafuasi ambao wapo tayari kwenda walipo " ulipo tupo"

  3. Hawana furaha au uhakika wa usalama wa maisha yao ya kisiasa, hapo walipo sasa.

  4. Ni wa pambanaji.

  Factors hizi zinawafanya kutengeneza bond , ama combination nzuri , kwa wale mashabiki wa mpira unaweza ifananisha na kikosi cha ushambuliaji cha timu ya Barcelona!

  Siasa ndivyo ilivyo!

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku