• Breaking News

  Oct 15, 2016

  Maadhimisho ya Nyerere Yafanyika Bila Familia ya Nyerere

  Maadhimisho ya miaka 17 ya kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Julius Nyerere yaliyofanyika jana mjini Bariadi mkoani Simiyu jana bila kuwapo wa familia ya mwasisi huyo wa Taifa.

  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka alisema Oktoba 5, mwaka huu Mama Maria Nyerere alikuwa miongoni mwa waalikwa katika sherehe hizo na mipango kwa ajili ya malazi yake na msafara ilikuwa imeandaliwa.

  Katika mipango ya awali, mama Maria na msafara wake alipangiwa kufikia katika nyumba za halmashauri ya mji wa Bariadi zilizoko eneo la Nyamuata kabla ya kuhamishiwa katika hoteli mpya ya Sumayi katikati ya mji wa Bariadi.

  Meneja wa hoteli hiyo, Mabula Mapolu alithibitisha ugeni wa Mama Maria kupangiwa kufikia hotelini lakini, baadaye walipewa taarifa kuwa ugeni huo usingefika na badala yake

  hoteli hiyo ikapangiwa wakuu wa mikoa na wilaya kutoka Zanzibar, ambao nao walilazimika kuondoka juzi kutii agizo la Rais John Magufuli la kuwataka kurejea kwenye vituo vyao vya kazi.

  Akizungumzia sababu za familia hiyo kutofika, mmoja wa watoto wa Mwalimu Nyerere, Madaraka

  Nyerere alisema yeye binafsi hakuona mwaliko wa familia kuhudhuria sherehe hizo, akisema huenda ulipokewa na mwana familia mwingine kwa kuwa familia yao ni kubwa.

  “Yawezekana mwaliko ulipokewa na mmoja wa wanafamilia kutokana na familia yetu kuwa kubwa. Lakini aliyeupokea akapata hudhuru na

  kushindwa kuhudhuria; Hii haimaanishi kuwa Serikali haikutoa mwaliko,” alisema Madaraka akiwa Butiama.

  Familia hiyo jana ilishiriki ibada maalumu katika Kanisa Katoliki Butiama ambayo pia ilihudhuriwa na viongozi kadhaa wa Serikali, wakiwamo Mkuu wa mkoa huo, Dk Charles Mlingwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo aliyetajwa kumwakilisha Rais John Magufuli pamoja na wakuu wa wilaya za mkoa wa Mara.

  Mbunge wa Afrika Mashariki, Shyrose Bhanji na mbunge wa Bunda, Ester Bulaya pia ni miongoni mwa waliohudhuria ibada hiyo.

  Mbali na maadhimisho ya kitaifa yaliyoambatana na sherehe za kuzima mwenge, ilifanyika ibada katika

  Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Yohana mjini Bariadi iliyoongozwa na Askofu wa Jimbo la Shinyanga, Liberatus Sangu.


  Askofu Sangu aliwataka viongozi wa Serikali

  kuyaenzi kwa vitendo aliyoyaacha Nyerere kwa kupiga vita na kukemea rushwa, ubadhirifu, ubaguzi wa kiitikadi, kidini, kikabila na maeneo huku kila mmoja akidumisha amani, utulivu.

  Aliwaomba Watanzania kila mtu kwa imani yake kushirika kumwombea Mwalimu Nyerere kutangazwa kuwa mwenye heri katika mchakato unaoendelea ndani ya Kanisa Katoliki.  Dk Shein

  Akihutubia taifa katika kumbukumbu hiyo, Rais wa Zanzibar, Dk Ally Mohamed Shein aliahidi kuwa Serikali itayaenzi yote yaliyoasisiwa na Mwalimu Nyerere akitaja ulinzi na usalama, amani, upendo, mshikamano na umoja wa kitaifa kuwa ni miongoni mwa hayo.

  Kiongozi huyo alisisitiza msimamo wa Serikali wa kutokubali msaada yenye masharti ya kutweza, kudhalilisha utu na uhuru wa Watanzania, badala yake aliahidi kuwa Tanzania itashirikiana na mataifa yote na kupokea misaada isiyo na masharti magumu.

  Akizungumzia uwezeshaji kwa vijana, Dk Shein alisema Serikali itaendelea kutekeleza sera ya kuweka mazingira bora na kuwawezesha vijana kuanzisha miradi ya kiuchumi kulingana na fursa zinazopatikana katika maeneo yao huku akikemea tabia ya baadhi ya vijana kushinda vijiweni bila kufanya kazi.

  Katika hotuba yake Dk Shein alisisitiza msimamo wa Serikali za Muungano na Zanzibar katika kupambana na ubadhilifu na rushwa ili kuboreshwa na kuimarisha huduma za kijamii katika nyaja zote.

  Kiongozi wa mbio za Mwenge, George Mbijima alitaja tishio la kiusalama kutokana na wahamiaji

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku