• Breaking News

  Oct 24, 2016

  MAALIM Seif Adai Kuna Njama za Kumpulizia Sumu

  Maalim Seif
  Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuna njama za kumkamata na kumpulizia sumu itakayomuua taratibu.

  Maalim Seif aliyezaliwa  Oktoba 22, 1943 katika Kijiji cha Nyali wilayani Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, amesema hayo wakati akisherehekea siku yake ya kuzaliwa.

  Mwanasiasa huyo mkongwe ametoa tuhuma hizo juzi mbele ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji, Baraza Kuu, viongozi, watendaji na wafuasi wa CUF.

  “Kwa taarifa za kuaminika, zipo njama za kunikamata, wanipeleke Dar es Salaam, kama walivyowafanyia masheikh. Waniweke katika chumba maalumu kidogo, kisha wanipulizie dawa hatimaye afya yangu izoroteshe afya taratibu na mwishowe nifariki dunia,” amedai Maalim Seif bila ya kutaja wanaotaka kumkamata

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku