Oct 16, 2016

Maalim Seif 'Kinachoendelea ni Mpango Ulioandaliwa wa Kuvuruga CUF'


Mwanasiasa Maalim Seif azungumzia mgogoro wa Chama cha CUF. Asema kinachoendelea ni mpango ulioandaliwa wa kuvuruga jitihada za chama hicho kudai haki Zanzibar “Nasema hiyo ya Profesa Lipumba ni ajenda iliyolenga kutuparaganya ili tuondoke katika mazingira na hima ya kutetea haki yetu iliyoporwa. Lakini msijali hiyo haitafanikiwa nasi tumefikia pazuri sasa,” alisema Seif

Alilaumu juhudi alizoziita za baadhi ya watu kutumia vibaya mamlaka kutaka kumzuia asiongee na wananchi licha ya kuwa umma unayo shauku kubwa ya kuhitaji kumsikiliza kila anapopita. “Najua zipo kila mbinu na hila za kutaka mimi nisiongee nanyi. Wenyewe mmeshuhudia hapa msikitini baada ya kubainika nakuja, lakini nasema mimi ni binadamu na kiongozi, ninayo haki ya kuongea na yeyote popote.Nitaongea na nitaongea popote pale,” alisema.


Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR