• Breaking News

  Oct 13, 2016

  MAJAMBAZI Wanne Walioua Polisi Wanne Mbagala, Wauawa

  Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewaua majambazi 4 na kukamata silaha ya jeshi hilo iliyoporwa atika tukio la ujambazi kwenye uvamizi wa Benki maeneo ya Mbande Mbagala ambapo polisi wanne waliuawa.

  Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Simon Sirro amesema majambazi hayo ndiyo waliohusika na mauaji ya polisi na kufanya matukio mbalimbali ya uhalifu katika maeneo mbalimbali nchini na kwamba waliuawa baada ya majibizano ya risasi na polisi katika pori la Dondwe mpakani mwa Chanika na Mkoa wa Pwani.

  Kamanda Sirro amesema jumla ya silaha 2 na risasi 24 na bomu moja lililotengenezwa kienyeji, vimekamatwa katika matukio tofauti jijini humo sambamba na kuwakamata 'Panya Road' 10 wenye umri wa miaka chini ya 18 wanojihusisha na matukio ya uporaji katika maeneo ya Mbagala Jijini Dar es Salaam.

  Vijana hao wenye umri chini ya miaka 18 wanaojihusisha na matukio ya uhalifu maeneo ya Mbagala walifikishwa mbele ya wanahabari ambapo Kamanda Sirro ameitaka jamii kuwalea watoto wao vizuri na kuendeleza ulinzi wa polisi jamii kwenye maeneo yao.

  Aidha Jeshi hilo pia limekamata shehena ya mafuta ya kula yenye madumu 453 kwa kukwepa kodi yenye thamani ya shilingi 14,296, 680 na mtambo bandia wa kutengeneza pombe aina ya Konyagi, rola 57 za viroba pamoja madumu sita yenye ladha ya kutengenezea kinywaji hicho.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku