Oct 16, 2016

Makamba Aagiza Watu Kuondolewa Mara Moja Katika Chanzo Cha Maji Morogoro

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira na Muungano, January Makamba amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, John Mgalula kuhakikisha kuwa ifikapo Novemba 30 mwaka huu watu wote wanaoishi na kufanya shughuli za kibinadamu katika chanzo cha maji cha Mambogo waondolewe haraka.

Waziri Makamba alitoa agizo hilo leo wakati alipotembelea chanzo cha maji cha Mambogo kinachotegemewa na wananchi wa Manispaa ya Morogoro mara baada ya kujionea uhalibifu unaoendelea kufanywa na wananchi hao na kusababisha maji kukauka.

Waziri huyo alimtaka mkurugenzi huyo kuwaondoa na kuwafikisha mahakamani wale wote waliochepusha maji kutoka katika chanzo hicho kwani wamekuwa wkaifanya hivyo kinyume na sheria, kanuni na taratibu zilizopo zinazokataza kufanyika kwa shughuli zozote za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji.Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR