Oct 14, 2016

Maradona Nusura Azichape na Veron

Mchezo mahsusi kwa ajili ya kuhamasisha amani ulioandaliwa na Papa Francis ulihusisha nyota kadhaa waliostaafu na ambao bado wanacheza akiwemo Ronaldinho, Francesco Totti, Edgar Davids, Hernan Crespo na Bojan Krkic.

Mchezajia nguli wa soka nchini Argentina, Diego Maradona na Juan Sebastian Veron ambao walikuwa kati ya wacheaji ambao walikuwepo mchezo huo ambao ulifanyika siku ya Jumatano nusra wazichape katika mchezo huo wa hisani uliofanyika jijini Rome, Italia.

Wawili hao walikuwa wakitupiana maneno mpaka kufikia hatua ya kutaka kushikana wakati wakielekea nje ya uwanja wakati wa mapumziko.

Maradona inaonekana hakufurahishwa na jinsi Veron alivyokuwa akimchezea ambapo ilibidi azuiwe na beki wa zamani wa kimataifa wa Brazil Cafu pamoja na watu wa usalama wakati akitaka kwenda kumvaa Veron

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR