• Breaking News

  Oct 24, 2016

  MBOWE: Makamanda Muelewe Kuwa Hii ni Awamu ya 5 Sio ya 4

  Kamanda wa anga na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Aikaeli Mbowe. Mapema leo ameandika jumbe zifuatazo kupitia ukurasa wake wa Twitter;


  =>Ambacho naomba Makamanda wenzetu muelewe ni jambo moja, hiki sio kipindi cha kawaida awamu ya tano sio awamu ya nne.

  => Demokrasia haiheshimiwi, Sheria haziheshimiwi, Katiba haiheshimiwi, Jeshi la Polisi limekuwa Mawakala wa CCM.

  => Tunakwenda Mahakamani,tunasema Kiongozi anaewaongoza watu, lakini hakuchaguliwa na watu amepachikwa na dola,hawezi kuwa Kiongozi halali.

  => Huyo Meya wao watakaefikiria wamempata mimi na imani hana baraka za wananchi, hana baraka za Mungu na sisi hatuna sababu za kumpa baraka.

  => Vyombo vya habari ambavyo huandika habari bila upendeleo kama Mwananchi,Tanzania Daima,Mtanzania, Mwanahalisi walizuiwa kuingia ndani.

  => Vyombo vya habari vilivyoruhusiwa kuingia ndani ni TBC ambao ni Mawakala wao, gazeti la Uhuru na Habari leo.

  => Walizuia vyombo hivi vya habari ili visishuhudie uhuni ulioendelea ndani, kulikuwa na askari wengi, wenye silaha nzito na mabomu.

  => Askari Wenye uniform na wasio na uniform,tunaliangamiza Taifa hili, tunasema Rais utaratibu huu na utamaduni huu aliouanzisha kuua.

  => Kuua demokrasia, analiletea Taifa hili madhara makubwa na maafa makubwa, Wananchi waliamua vyama vinavyounda UKAWA viongoze Kinondoni.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku