• Breaking News

  Oct 30, 2016

  Mkurugenzi Mvomero, Morogoro kitanzini kwa shilingi milioni 120

  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro Florent Kyombo, ametuhumiwa na baraza la madiwani kuwa anatumia vibaya madaraka yake kutokana na kufanya ubadhirifu wa fedha za halmashauri hiyo kiasi cha shilingi milioni 120.

  Licha ya tuhuma hiyo, mkurugenzi huyo anatuhumiwa pia kutoitisha vikao vya kisheria, fedha kutumika huku kukiwa hakuna vikao, pamoja na kukusanya mapato mengi huku hayajulikani yanakoenda.

  Kulingana na tuhuma hizo mkurugenzi huyo amekanusha tuhuma hizo akidai kuwa sio za kweli, bali madiwani hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa halimashauri Jonas Van Zeelanda, na Mbunge Murad Sadiq ndio waliendesha vikao vya kisheria vya halimashauri hiyo kwa siku tatu kwa kikao cha masaa 6 kinyume cha sheria, wakati mwenyekiti na Mbunge wakijilipa fedha za mafuta ya gari shilingi 144,000 kwa kila kikao.

  Pia Mkururugenzi huyo amedai kuwa alikabidhiwa ofisi na deni la jumla ya zaidi ya Shilingi Bilioni Moja, pesa zote hizo zikiwa zimetumika kinyume cha sheria, fedha za hospitali zaidi ya shilingi Milioni 200 za kujengea hospitali zimetumiwa kinyume cha sheria, ikiwa pesa zote wamelipana posho na kuidhinisha matumizi bila kufuata taratibu.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku