• Breaking News

  Oct 15, 2016

  Moto Wawaka Kashfa Kontena 100 Bandari

  SIKU moja baada ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, kusema kontena 100 zimeondolewa Bandari ya Dar es Salaam bila kukaguliwa na Shirika la Viwango (TBS), moto kuhusiana na suala hilo umezidi kuwaka.

  Hali hiyo imejidhihirisha kutokana na taarifa kuwa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) haikuhusishwa vya kutosha katika utoaji wa taarifa sahihi juu ya suala hilo huku TBS wakidai kuwa hadi kufikia jana, tayari wafanyabiashara 10 walishajitokeza kwao kwa nia ya kutoa maelezo.

  Akiwasiliana na Nipashe jana, Mkurugenzi Mkuu wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko, alielezea kushangazwa na taarifa zilizoelezwa kuhusiana na kontena hizo.

  Aidha, Kakoko alisema hali hiyo ya kutolewa maelezo bila kutaka taarifa kwao ni sawa na ‘kukwepa kupata taarifa sahihi kutoka sehemu sahihi’.

  1 comment:

  1. Tunasema kama wajanja wajanja wanataka kutumia Fursa ya Bakhresa Wamekose na tutawashughulikia. Kodo Kodi ni lazima na ni pato la Taifa.. TUTAWATUMBUA TENA KWA NGUVU ZOTE.

   ReplyDelete

  Siasa

  Michezo

  Udaku