• Breaking News

  Oct 23, 2016

  Mr Nice aeleza kwanini anakubalika Kenya

  Mwanamuziki, Lucas Mkenda ‘Mr Nice’ amesema ukongwe wake kwenye muziki ndiyo kitu ambao kinampatia mashavu zaidi nchini Kenya.

  Akiongea na Bongo5 Alhamisi hii, Mr Nice amesema Kenya ni sehemu pekee ambazo anaweza kufanya show nyingi bila mashabiki kumchoka.

  “Najivunia kuwa rafiki namba moja wa Wakenya,” alisema Mr Nice. “Hiyo ni silaa yangu kubwa katika muziki wangu, kwa hiyo labda ni kwa sababu tayari tumeshatengeneza chemistry nao toka naanza kufanya muziki,”

  Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na albamu yake ya Kioo, hivi karibuni alijaza umati wa mkubwa katika show yake iliyofanyika katika club moja huko nchini Kenya.

  Muimbaji huyo ijumaa hii atakuwa mjini Kisumu na Jumamosi atakuwa katika jiji la Nairobi maeneo ya Embakassy katika muendelezo wa show zake.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku