• Breaking News

  Oct 30, 2016

  Msajili Korti Kuu Ajitoa Kesi ya Babu Tale


  Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Projest Kahyoza amejitoa kusikiliza shauri linalowakabili wakurugenzi wa kampuni ya Tiptop Connections ya jijini Dar es Salaam, Hamis Shaaban maarufu Babu Tale na ndugu yake, Idd  Shaaban.

   Kahyoza alifikia uamuzi huo juzi, siku aliyopanga kutoa maelekezo maalumu kwa wadaiwa hao. Hata hivyo, mlalamikaji Sheikh Hashim Mbonde alimuomba ajitoe kwa madai kuwa hana imani naye.

  Katika shauri hilo, Babu Tale na nduguye wanatakiwa kujieleza ni kwa nini wasifungwe jela kwa kushindwa kutekeleza amri ya Mahakama hiyo.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku