• Breaking News

  Oct 25, 2016

  MTOTO wa Mbunge Akamatwa Kwa Tuhuma za Ujangili....

  Mtoto wa Mbunge wa Mbarali, Haroon Mulla (CCM), ametiwa nguvuni kwa tuhuma za kukutwa na meno ya tembo pamoja na nyama ya pori kinyume cha sheria.

  Tukio hilo lilitokea jana wilayani Mbarali ambapo mtoto wa mbunge huyo alikamatwa na shehena ya meno ya tembo pamoja na nyama hiyo ambayo haijajulikana kiasi chake.

  Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya vyombo vya dola mkoani Mbeya vimesema kuwa baada ya tukio hilo maofisa wa Serikali pamoja na askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) walimtia mbaroni mtu huyo na kumhoji kwa lengo la kubaini mtandao wa ujangili anaoshirikiana nao.

  Chanzo hicho kilisema kuwa familia hiyo imekuwa ikihusishwa na tuhuma za ujangili pamoja na kufanya biashara ya meno ya tembo kwa miaka mingi.

  Alipotafutwa Meneja Mawasiliano wa Tanapa, Pascal Shelutete ili kupata ufafanuzi wa tukio hilo akiri kukamatwa kwa mtoto huyo wa mbunge na kueleza kuwa wanaendelea na uchunguzi.

  “Ni kweli tunamshikilia mtuhumiwa na tunaendelea naye na uchunguzi na ukikamilika tutatoa taarifa kwa umma,” alisema.

  Mbunge huyo alitafutwa ili kuzungumzia taarifa za mtoto wake kuhusishwa na mtandao wa ujangili, hakuweza kupatikana kutokanana simu yake ya mkononi kuita bila kupokewa.

   – Mtanzania

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku