Oct 19, 2016

Mtoto wa Mfalme Saudia Arabia Anyongwa

Mtoto wa kifalme wa Saudi Arabia (prince) amenyongwa baada ya kumpiga risasi na kumuua mtu kwenye ugomvi uliotokea miaka miwili iliyopita kwenye mji mkuu, Riyadh.

Prince Turki bin Saud al-Kabir alinyongwa kwenye mji mkuu. Hakuna taarifa za jinsi alivyonyongwa lakini wahalifu wengi huchinjwa. Mwana mfalme huyo anakuwa mtu wa 134 kunyongwa mwaka huu, kwa mujibu wa orodha iliyokusanywa na shirika la habari la AFP.

Lakini ni nadra sana mwana familia ya kifalme kupewa adhabu hiyo. Familia ya mhanga ilikataa kupewa fedha kama mbadala wa adhabu ya kifo kwa mtuhumiwa.

Kesi nyingine ya mwana familia ya kifalme kuuawa ni pale Faisal bin Musaid al Saud, alipomuua mjomba wake, King Faisal, mwaka 1975.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR