• Breaking News

  Oct 23, 2016

  Mwanamuziki Ray C Aamua Kuingia Studio

  Ukimya wa muda mrefu wa Rehema ‘Ray C’ Chalamila’ uko mbioni kuzimwa kwa kishindo. Ni kwasababu mwanamuziki huyo mkongwe, ameingia studio za Wanene Entertaiment jijini Dar kurekodi kazi mpya.

  Muimbaji huyo ambaye kwa muda mrefu amekuwa akipambana na uraibu wa madawa ya kulevya, amepata mshirika mjuzi wa kumuongoza katika mrejeo wa nguvu – Damian Soul.

  “God is good all the time…With my beautiful sister @rayc1982 in the kitchen cooking together with @salthak_tale ..something amazing is coming out,” ameandika Damian kwenye picha aliyoiweka Instagram.

  “Happy moment sambamba na my lovely soul sister @rayc1982 in our kitchen @wanenestudios @sarthak_tale …It’s all about love & sharing,” ameongeza kwenye picha nyingine.

  Naye Rehema amepost kipande kifupi cha video akiwa na wawili hao na kuandika, “Cooking some delicious food in the studio.”

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku