• Breaking News

  Oct 4, 2016

  NAIBU Spika Dk. Tulia Katangaza Kuiendeleza Jadi

  Najua kuna watu wangu wana love ya kutosha pale wanaposikia suala la burudani, yes..! kama na wewe ni mmoja wapo basi hii si yakukosa, Naibu spika Dk. Tulia Ackson ametuandalia tamasha la ngoma za jadi litakalofanyika Tukuyu mkoani Mbeya kuanzia tarehe 7 hadi 8 mwezi October 2016.

  Dk. Tulia amesema…
  ’Nimeandaa tamasha la ngoma za jadi litakalofanyika Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya kuanzia October 7 hadi 8 2016 huku likiwahusisha wananchi mbalimbali wakiwemo wakazi wa Mbeya‘
  ‘Wazo hili nilikuwa nalo zamani lakini sasa nimepata fursa ya kufanya hivyo huku lengo likiwa ni kuzifanya ngoma za jadi zijulikane kwamaana zimekosa umuhimu kutokana na watu wengi wa vijijini kukimbilia mijini huku wakisahau tamaduni zao‘ –Dk. Tulia Ackson
  ‘Kwa washiriki waone hiyo kama moja ya fursa za kiuchumi kwakuwa hadi sasa nimetafuta wafadhili ili baadhi ya vijana wakapate nafasi ya kujiendeleza kimasomo katika chuo cha Bagamoyo, nataraji watu wa Rungwe na Kyela watajionea tamaduni zetu mbalimbali‘ –Dk. Tulia Ackson
  ‘Hizi ni tamaduni za Kinyakyusa ambazo nimepanga kuanza nazo lakini baadae tukijaaliwa tutaenda katika tamaduni za makabila mengine ikiwemo nchi nzima, katika tamasha kama hili lengo kubwa ni kukuza utamaduni kwamaana hiyo kila mtu ataingia na kushiriki bure‘ –Dk. Tulia Ackson

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku