• Breaking News

  Oct 28, 2016

  Napongeza Maoni Gazeti la Mtanzania kuhusu Habari ya Tukivitaka vyama vingi tuheshimu utamaduni wake

  Katika gazeti la Mtanzania toleo la jumatano October 26 2016, Sehemu ya maoni ya mhariri ilikuwa na kichwa kikisomeka "TUKIVITAKA VYAMA VINGI TUHESHIMU UTAMADUNI WAKE". nimeguswa na maoni ya mhariri kwa sababu nyingi sana, mhariri mambo mengi aliyotaja anglau kwa ufupi ni kuwanyima vyama shindani sehemu za kufanyia mikutano mwaka jana wakati wa uchaguzi e.g uwanja wa taifa na Jangwani, ukiukaji wa makusudi wa CCM kama kupitisha muda wa kufanya mikutano, kuwawekea restrictions ya kutembea mahali fulani wagombea wa vyama shindani wakati wa uchaguzi, figisu za uchaguzi wa mameya wa kinondoni na Ubungo, n.k. mhariri anamaliza kwa kushauri kwamba kuwapo kwa mfumo wa vyama vingi si kuwapo kwa vyama tu bali pia kuheshimu misingi yake, haki na utamaduni wake wa kushindanisha hoja bila kupigana.

  Mimi binafsi nilitamani mhariri aendelee kudadavua zaidi lakini kwa kuwa safu yake ni fupi aliishia hapo. Mimi nitaongezea alipoishia, Ni takribani miaka ishirini toka tuingie katika mfumo wa vyama vingi lakini watu na taasisi bado zinaonyesha "ushamba" wa kisiasa wa hali ya juu, ushamba huu unaweza kuwa wa kujitakia "willful ignorance" au wa mifumo mibovu tiliyojiwekea. nikitoa mifano ya yanayotokea sasa hivi taratibu na sheria tulizojiwekea zimekuwa hazifuatwi, madiwani kila siku wanawekwa ndani na wakuu wa wilaya na mikoa kumpendezesha "mkulu" maana ndo imekuwa ngazi ya kupanda vyeo, polisi wamekuwa wakitumika ndivyo sivyo. Miradi mbalimbali ya maendeleo haipelekwi katika sehemu amabazo UKAWA walishinda ili kuwakomoa. Kwa mfano mkoa wa Arusha mkuu wa mkoa amesimamisha shughuli zote za maendeleo na ndiye anafanya kazi kama mkurugenzi. Mkurugenzi aliyepo amebaki kujipendekeza na kuonekana kama bulldog, ukiukaji huu wa taratibu si tu unaonyesha ignorance ya mfumo wa vyama vingi bali pia unakiuka haki stahiki za watu ambao wanalipa kodi bila kujali itikadi. Kwa maana nyingine tunaendesha nchi kwa ubaguzi wa maeneo kisa hawaamini kile ambacho wewe unaamini, utamaduni huu ni utamaduni wa kigaidi, magaidi ndo wanataka lazima uamini wanachoamini wao ndo utaweza kuishi. Kma hivyo ndivyo watu wataupinga kwa nguvu zote ugaidi huu.

  Ningeweza kuendelea zaidi lakini sitaki kuwachosha wasomaji labda na mimi nitoe maoni yangu kwamba tunahitaji kuanza upya mfumo wa vyama vingi, watu na taasisi nyingi zinahitaji kufanyaiwa capacity building. Kwa bahati mbaya wakati tunaanzisha vyama vingi taasisi nyingi hazikufanyiwa capacity building as a result hawajui namna ya kufanya kazi under multi party democracy. Kwa mfano jeshi la polisi linahitaji kufundishwa upya kwamba chini ya mfumo wa vyama vingi wanatakiwa kufanya kazi namna gani, wakuu wa mikoa na wilaya wanatakiwa wa-behave nanma gani n.k

  Nawasilisha wakuu

  Emalau

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku