• Breaking News

  Oct 22, 2016

  NDUGAI Awachana Wafanyakazi wa Serikalini "Acheni Kuota Hela ya Serikali, Mtatumbuliwa"

  Spika wa Bunge, Job Ndugai, amewatahadharisha wakuu wa idara na madiwani wa halmashauri nchini kujiepusha na masuala ya wizi na kwamba kuwataka kutothubutu kuota hela ya serikali.

  Ndugai ametoa tahadhari hiyo wakati akizungumza na madiwani katika kikao cha baraza cha halmashauri ya wilaya ya Kongwa.

  “Niwaombe sana wataalamu, nyakati zimebadilika sana na hata nyie nyie mnaona,” alisema. “Kile kidogo kilichokuja kwaajili ya maendeleo kitumieni kwaajili ya maendeleo, usilale unaota kwamba utachakachua utaiba sehemu fulani ya hiyo hela, acha kabisa kuota hela ya serikali – kwamba eti utaweka mfukoni na ukaishi, utatumbuliwa tu, ndo hali halisi na ukweli wenyewe,” alionya.

  “Madiwani ni hivyo hivyo, anzisha miradi yako, simamia mambo yako, usitegemee kwasababu wewe ni diwani ikaletwa hela ya kujenga darasa sijui zahanati ukategemea utaweka mrija wako pale ili kuishi. Hizo age zimeshapita, enzi zile za kujineemesha wewe binafsi kwa ujanja ujanja zimepita, naomba tulikubali hili jambo.”

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku