• Breaking News

  Oct 8, 2016

  Ofisi ya Hifadhi ya Serengeti yateketea kwa moto


  J`engo la utawala la ofisi ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti(Fort Ikoma) wilayani Serengeti Mkoa wa Mara limeteketea kwa moto leo Jumamosi na vifaa mbalimbali vya ofisi .

  Mhifadhi mkuu wa hifadhi hiyo, William Mwakilema amesema tukio hilo saa 5 asubuhi leo hii.

  Mwakilema alisema kuwa moto huo umeanzia kwenye chumba cha wataalam wa tiba za wanyama na kusambaa jengo lote na kuteketeza paa na vitu vingi vya ofisi,hata hivyo chanzo chake hakijajulikana.

  "Katika chumba hicho kuna mafriji ya madawa, chanzo hakijajulikana mpaka sasa na pia hasara iliyosababishwa na moto huo haijajulikana...kwa ujumla ni hasara Kubwa kwa Kuwa jengo hilo limeteketea kabisa na lina ofisi nyingi ikiwemo idara ya fedha ,"alisema .  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku