• Breaking News

  Oct 29, 2016

  Ole Sendeka, Walipeni Uhuru Mishahara Kwanza, Achaneni na Zitto na Lowassa

  Nimesikiliza Video inayosambaa kwa Kasi Mtandaoni inayomuonyesha Karani na Msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka akiwatuhumu Edward Lowassa wa CHADEMA na Zitto Kabwe kiongozi wa chama wa ACT WAZALENDO.

  pamoja na kumsikiliza zaidi ya mara tatu lakini sipata kuelewa alikuwa anajaribu kumaanisha nini.?.

  na kama ndio msemaji wa chama kinachotawala nchi anaweza kuwa na kiwango cha uelewa wa aina ya Sendeka basi sitashangaa kuona nchi ya Viwanda ikipatikana mwaka 3000.

  sendeka anawataka LOWASSA na Zitto wamsifie Magufuli, hajasema kwa Lipi?,

  Sendeka anamtaka Zitto aisifie CCM, ili apate nini?, kwanini Sendeka asiendelee tu kuisifia CCM inayompa Ugali baada ya Kushindwa ubunge Simanjiro?.

  Zitto Kabwe sio KARANI wa CCM kama Sendeka, zitto ni Kiongozi wa chama cha siasa kinachojitegemea, ni chama kama anachokiwakilisha Sendeka chenye mwenyekiti wake MAGUFULI.

  Zitto Kabwe sio Msemaji wa Serikali ya CCM, Zitto na ACT WAZALENDO tumeweka Wazi kabisa, kwamba Tunaupinga Ujinga popote ulipo, Ikiwa Ujinga wa CCM unashabihiana na ulio nje ya CCM tutaupinga kwa nguvu ileile.

  sio wajibu wa ACT kuisifia CCM, MAGUFULI na SERIKALI yake, tutaipongeza itakapofanya vema na tutaikosoa itakapoboronga. sisi kwetu nyekundu ni nyekundu na njano daima huwa njano.

  Sendeka aliyekuwa analilia Demokrasia, Utawala wa Sheria na Usimamizi wa Sheria za Manunuzi leo ameufyata kabisa.

  #Sendeka aliyesimama Bungeni Kipindi cha Richmond na Kumshambulia Lowassa kwa kutokufuata sheria za manunuzi, leo anamshangilia Magufuli kwa kufanya madudu yaleyale - kweli njaa haina Baunsa.

  kwanini umekubali kuwa Mnafiki kiasi hicho?, kwanini usikisaidie chama chako cha mapinduzi kutatua kero za watumishi wake?.

  SENDEKA, nakukumbusha kuwa Pamoja na CCM kupokea RUZUKU ya MILIONI 960 lakini leo ni mwezi wa TISA mfululizo hakijawalipa Mishahara WAANDISHI NA WATUMISHI wa GAZETI LA UHURU.

  Mwenyekiti wenu wa chama alikwenda akaahidi kuwalipa mwisho wa mwezi uliopita, lakini mpaka leo wanalala na njaa vijana wa watu.

  Sendeka wasemee wafanyakazi wa UHURU walipwe mishahara yao achana na Zitto, achana na LOWASSA.

  Sendeka Msaidie Mwenyekiti wako Kujenga hata Msingi wa kiwanda cha Rangi za Kucha, achana na Zitto achana na Lowassa.

  Sendeka wasaidie watumishi wa Serikali wawezeshwe, leo tunavyozungumza, baadhi ya Ofisi za umma hazina hata mafuta ya magari ya kazi, wote wanaogopa hata kuomba pesa za uendeshaji wa ofisi, wanaishia kusoma magazeti tu,

  SENDEKA, Bunge limeshindwa kutoa Photocopy Muswada wa Sheria ya Habari kwa kukosa pesa za kufanyia kazi yake, umekaa kimya.

  SENDEKA isaidie CCM kuueleza Umma lini SERIKALI YA MAGUFULI itaacha kuwalipa MATAPELI WA IPTL milioni 400 kila siku ama wamezalisha umeme au hawajazalisha, achana na Lowassa achana na Zitto.

  SENDEKA wasaidie kuwajuza wanachama wa CCM kuhusiana na Mali za chama hasa mtambo wa kuchapia magazeti mliouuza kwa kupima Kilo kama SCREPA, Achana na Lowassa achana na zitto.

  Tunaikosoa CCM, tunaikosoa Serikali ya CCM, Tutamkosoa Magufuli kwa Hoja na Tutampongeza kwa kila zuri atakalofanya.

  SENDEKA na CCM hamna mamlaka ya kuwafundisha ama kuwachagulia wapinzani nini cha kufanya ama nini cha kusema wakati gani na wapi.

  Ndimi
  Habib Mchange
  Katibu wa Bunge na Serikali za Mitaa
  ACT WAZALENDO

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku