• Breaking News

  Oct 19, 2016

  P-Funk atangaza kumpata msichana wa kwanza kumsainisha Bongo Records

  Kwa muda mrefu, producer mkongwe wa Bongo Flava, P-Funk Majani alikuwa akizungumza nia yake ya kupata wasanii wa kike kwaajili ya kuwasainisha Bongo Records.

  Na sasa ametangaza kumpata msichana wa kwanza atakayemwagika wino kuwa chini ya usimamizi wa label yake kongwe. Anaamini kuwa msichana huyo atafanya mambo makubwa.

  “I finally found the perfect female artist to sign to Bongo Records. She’s gonna take over the music industry by storm,” ameandika Majani kwenye picha ya msichana huyo aliyoiweka Instagram.

  “What do you think, does she rap or sing,” amehoji.

  Hivi karibuni Majani alisema anatarajia kutambulisha vipaji vipya takriban vinane vitakavyokuwa chini ya label yake.

  Mpango huo aliutambulisha takriban miaka miwili iliyopita na kupata wasanii lakini alikosa muda wa kuendelea baada ya kupata majukumu ya kampuni ya CMEA.

  Na sasa amesema ameshakutana na wasanii hao tena na kuongeza wengine tayari kwa kuufufua mradi huo.

  “Tuseme wako kama nane kwahiyo sasa hivi ndio tupo studio tunajifua, kila mmoja anapiga kazi tatu tatu then tutawaalika watu wa media, watu wa industry, tutakaaa tutakagua zile nyimbo na nyinyi mtapata nafasi sasa ya kuchagua single zao ambazo sasa tutainvest, tutaingia kwenye videos na tutazazimarket zile.”

  Alidai kuwa bado anaendelea kusaka vipaji zaidi na kwamba angependa kupata wasanii wa kike zaidi.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku