• Breaking News

  Oct 21, 2016

  PAUL Makonda Ajiandaa Kupambana na Magenge ya Wahalifu Dar

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema ofisi yake inaanziasha operesheni maalum kwa ajili ya kupambana na magenge ya wahalifu ambayo yaibuka hivi  karibuni.

  Akizungumza leo (Ijumaa) kabla ya uwekaji jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa hosteli za wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Makonda amesema hiyo ndiyo changamoto inayoikabili jiji la hili.

  Makonda ambaye amesema hayo wakati akitoa salamu kwa Rais John Magufuli anayetarajia kuweka jiwe hilo muda mfupi kuanzia sasa amesema operesheni hiyo inalenga kushughulikia magenge ya wahalifu hao ambao wamekuwa wakidhuru wananchi na kupora mali zao.


  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku