• Breaking News

  Oct 24, 2016

  POLISI Lawamani Kifo cha Mtuhumiwa Wizi wa Kuku

  KITUO cha Polisi Mapinga wilayani hapa, kimeingia lawamani baada ya kudaiwa kusababisha kifo cha mkazi wa Kerege, Mohamed Ngatipura (43), aliyekuwa akishikiliwa kituoni hapo kwa tuhuma za wizi wa kuku.


  Kaka wa marehemu huyo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kerege, Said Ngatipura, aliliambia Nipashe mwishoni mwa wiki kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 15, mwaka huu.

  Ngatipula alisema siku ya tukio hilo, mdogo wake aliondoka nyumbani kwao muda wa mchana akiwa mzima, lakini majira ya jioni walipigiwa simu kuwa anashikiliwa katika Kituo cha Polisi Mapinga kwa tuhuma ya wizi wa kuku.

  "Baada ya taarifa hizo, mdogo wangu mwingine, Yahya Ngatipura na wenzake, walikwenda hadi kituoni, lakini hali waliyomkuta nayo ilikuwa si nzuri kutokana na kusumbuliwa na shinikizo la damu. Hivyo ikabidi wamuombee dhamana ili wampeleke hospitali, lakini askari waliokuwapo walikataa. Ndipo waliponifahamisha mimi ikabidi niende kituoni hapo," alidai Ngatipura.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku