• Breaking News

  Oct 9, 2016

  Polisi na TRA Wakamata Shehena ya Bidhaa Mbalimbali za Magendo Ambazo zinadaiwa Kuingizwa Nchini

  Polisi kwa kushirikiana na maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania - TRA- Mkoa wa Mara, wamekamata shehena ya bidhaa mbalimbali za magendo ambazo zinadaiwa kuingizwa nchini kwa njia ya magendo kupitia mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Sirari wilayani Tarime mkoani Mara.

  Meneja wa TRA mkoa wa Mara,  ERNEST NKANGAZA  ameiambia ITV kuwa bidhaa hizo zikiwemo galoni zenye  mafuta ya taa Lita zaidi ya 2,725,Diseli  Lita 960, Mifuko ya Plastiki ambayo imepigwa marufuku kuingizwa nchini pamoja Pipi na Dawa za Binadamu ambazo  zimekamatwa katika kijiji cha Maburi wilayani Serengeti.

  Amesema maafisa wa TRA walipata taarifa kuhusu gari yenye namba za usajili T881 BDE ambayo imeandikwa ubavuni AMOS .J.  BUHEMBWE ikiwa imebeba bidhaa hizo na waliweka mtego katika makutano ya Barabara ya Makutano ya Musoma-Mwanza na saa saba usiku gari hilo lilipofika eneo hilo na dereva wake aliamuliwa kusimama na kukaidi na kuliondoa kwa mwendo kasi hivyo kufukuzana hadi kijiji cha Maburi walipolitelekeza.

  Amesema baada ya upekuzi kufanyika wamebaini kuwa bidhaa hizo zenye thamani ya Mamilioni ya shilingi zilingizwa nchini bila kulipiwa kodi mbalimbali za Serikali.

  Kwa sababu hiyo meneja huyo wa TRA mkoa wa Mara amesema hivi sasa gari hilo na bidhaa zote zimehifadhiwa katika ofisi ya TRA wilayani Serengeti na kuwataka wamiliki wa gari na bidhaa hizo kujitokeza kulipa kodi hiyo kabla ya hatua nyingine za sheria kuchukuliwa dhidi yao.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku