• Breaking News

  Oct 30, 2016

  Polisi Yamzuia Maalim Seif, Yamlinda Lipumba

  Askari wa Jeshi la Polisi akimpigia saluti Profesa Ibrahim Lipumba ambaye ni Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na ofisi ya Msaijili wa Vyama vya Siasa nchini baada ya kiongozi huyo kumaliza kufanya usafi katika eneo la Buguruni jijini Dar es Salaam jana.

  Tanga. Wakati Polisi ikizuia mkutano mkuu maalumu wa CUF uliopangwa kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad mjini hapa jana, mwenyekiti anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba alifanya usafi Soko la Buguruni, Dar es Salaam huku akilindwa na jeshi hilo.

  Lipumba alifanya kazi hiyo akitekeleza agizo la Rais John Magufuli la kufanya usafi Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi.

  Msemaji wa CUF, Abdul Kambaya alisema haoni kama ni jambo la ajabu kwa Lipumba kufanya usafi wakati akilindwa.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku