• Breaking News

  Oct 1, 2016

  PROF. Lipumba Atengua Uteuzi wa Wakurugenzi na Manaibu wa CUF

  PROF. Lipumba 
  Mwenyekiti wa Chama Cha wananchi CUF anayetambuliwa na ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa, Profesa Ibrahim Lipumba ametengua uteuzi wa wakurugenzi na manaibu wao sita kwa kile alichokiita ni kutokana na changamoto zinazokikabili chama hicho.

  Wakurugenzi waliotenguliwa uteuzi wao ni pamoja na Mkurugenzi wa Uchumi na Fedha, Joran Bashange, wa Mambo ya Nje Ismail Jussa Ladhu, Ulinzi na Usalama Mustafa Wandwi, na Haki za Binadamu na Sheria Kulthum Mchuchuli.

  Pia Prof Lipumba ametoa siku moja kwa wafanyakazi wote wanaofanya kazi ofisi za CUF kwa kujitolea,kufika kesho Ofisini Buguruni kama wanataka kuendelea kufanya kazi nae,na wale ambao watakaidi kipufika,basi wajihasabie kuwa ndio wamejifukuzisha ktk nafasi zao

  Meanwhile;Habari za watu wa karibu na Prof wanasema ameendelea kulala na kushinda ndani ya Ofisi za CUF-Buguruni bila kutoka nje wala wala mbali na eneo la ofisi hizo.Ni mwendo wa kulala na kuamka ndani ya viunga vya Ofisi Buguruni.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku