Oct 14, 2016

Rais wa Nigeria Amjibu Mkewe...Adai Mkewe ni was Kwake Jikoni na Chumbani na si Vinginevyo


Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amejibu onyo kutoka kwa mkewe ambaye alikuwa ametahadharisha kwamba hatamuunga mkono uchaguzi mkuu ujao iwapo hatafanya mabadiliko serikali.

Bi Aisha, kwenye mahojiano na BBC, alikuwa amedokeza kwamba mumewe amepoteza udhibiti wa serikali.

Bw Buhari kwa sasa yumo kwenye ziara rasmi nchini Ujerumani na kwa mujibu wa shirika la habari la AP, amemjibu mkewe wakati wa kikao cha wanahabari akiwa pamoja na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel.

"Sijui mke wangu ni wa chama gani, lakini najua yeye ni wa kwangu jikoni na sebuleni na chumba hicho kingine," amesema Bw Buhari.

Kwa mujibu wa AP, kiongozi huyo aliyeingia madarakani mwaka jana amesema pia kwamba na ujuzi na uzoefu zaidi ya mkewe katika siasa.

"Kwa hivyo, nina ujuzi kushinda yeye na watu wengine wa upinzani, kwa sababu mwishowe nilifanikiwa. Si rahisi kuridhisha vyama vyote vya upinzani nchini Nigeria au kushiriki serikalini."


Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR