Oct 22, 2016

RIAS Magufuli Amteua Profesa Lema Kuwa M/kiti wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tz (TAA)

Rais John Magufuli,amemteua Profesa Ninatubu Lema kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).

Profesa Lema anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Lambert Ndiwaita aliyefariki dunia Agosti 20, 2015.

Taarifa iliyotolewa leo (Jumamosi) na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi huu umeanza tangu Oktoba 20, 2016.

Profesa Lema ni Profesa Mshiriki Usimamizi wa Ujenzi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR