Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, aliyeamuru Hamis Sengo, mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Shilala kudeki darasa mbele ya wanafunzi aigomea CWT kuomba msamaha.

Mkurugenzi huyo aliamuru mwalimu huyo adeki darasa baada ya kufanya ziara shuleni hapo na kukuta madarasa machafu

Mkurugenzi Mwaiteleke akiwa ameambatana na maofisa wengine wa serikali ngazi ya wilaya hiyo, alifika shuleni hapo majira ya jioni na kumuita mwalimu (Sengo) ili aeleze kwanini madarasa ni machafu na kumtaka kudeki kitendo kilichotekelezwa na mwalimu huyo bila kupinga.


Post a Comment

 
Top