• Breaking News

  Oct 31, 2016

  Saluti ya Polisi Kwa Prof Lipumba Yazua Gumzo

  Suala la polisi kumpigia saluti mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Profesa Ibrahim Lipumba limezua mjadala baada ya kuonekana kuwa si mmoja wa viongozi wanaopaswa kupata heshima hiyo kisheria.

  Juzi, Polisi alionekana akimpigia saluti Profesa Lipumba katika eneo la Buguruni alipokwenda kufanya usafi. Kitendo hicho kimeibua mjadala mitandaoni, watu wakihoji uhalali wa mwanasiasa huyo kupewa heshima hiyo.

  Juni 2005, aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Kapteni John Chiligati alipokuwa akijibu swali la aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu, Salome Mbatia alibainisha maana ya saluti na makundi ya watu wanaostahili kupigiwa saluti na askari.

  Chiligati alisema saluti ni kitendo kinachofanywa na askari kwa maana ya kutoa salamu kwa ishara yenye kuonyesha heshima. Pia, alisema saluti ni njia mojawapo ya kuonyesha heshima na utii kwa kiongozi mkuu kwenye asasi za kijeshi.


  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku