Oct 10, 2016

Serikali: Tumetenga Sh. Bilioni 85 Kupunguza Deni la MSD. Uhaba wa Chanjo Sasa Umetatuliwa...

Kwa Ufupi, Taarifa Inasema:

=> Taarifa kuwa kuna upungufu mkubwa wa dawa katika Bohari Kuu ya Dawa si za kweli

=> Suala la Afya ni kipaumbele kwa Serikali ya Awamu ya Tano

=> Hali ya upatikanaji wa dawa kwa sasa iko vizuri. Zipo antibiotics muhimu kama Amoxycillin, Ciprofloxacin, Cotrimoxazole na Doxycycline.

=> Aidha, taarifa inabainisha kuwa dawa za maumivu kama Paracetamol, Asprin na Diclofenac zipo za kutosha.

=> Taarifa inaongeza kuwa kuna dawa za Kifua Kikuu, Ukoma na zile za kufubaza makali ya UKIMWI(ARVs) zipo.

=> Chanjo za watoto na wajawazito - kweli kulikuwa na uhaba miezi 2 iliyopita lakini sasa zipo.

=> Wiki iliyopita, serikali imenunua na kupokea dozi milioni 2 za chanjo ya Kifua Kikuu(BCG) na Dozi milioni 1.2 za Polio na zinasambazwa ktk vituo vya afya nchini.

=> Hakuna haja ya bajeti ya dharura kwa hili.

=> Zimeshatengwa Sh. Bilioni 85 kulipa deni la MSD lililokuwa likidaiwa.

=> MSD haitapatiwa mshindani, itakuwa ni kurudufisha (duplication) majukumu.Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR